
Tanzania ni nchi yetu ambayo imebarikiwa kuwa na vivutio vingi na tunapozungumzia vivutio hivyo ni pamoja na hifadhi za taifa zinazopatika hapa nchini.
Leo katika katika blogu yetu pendwa Turism in Tanzania tunakuletea miongoni mwa hifadhi za taifa ambazo hupatikana hapa nchini zenye vivutio vya kustaabisha zaidi, Hifadhi hii ya Kisiwa cha Saanane ni hifadhi iliyoanzishwa kama bustani ya kwanza ya wanyama mnamo mwaka 1964. Lengo la kuanzishwa kwake lilikuwa ni kuhamasisha uhifadhi na kuelimisha jamii.
Ni dhahiri kuwa wengi tunaweza tukawa tunajiuliza kuhusu jina la hifadhi hii na ni kwanini iliitwa Saanane, lakini ukweli ni kwamba jina la hifadhi hii lilitokana na mwanzilishi wa bustani aliyeitwa Saanane Chawandi.
Kati ya mwaka 1964 na 1966 wanyama mbalimbali walihamishiwa katika kisiwa hiki, wanyama hao ni pamoja na mbogo, digidigi, tembo, pofu, pongo, swala pala, ngiri, pundamilia, twiga, nungunungu n.k.
Na inaelezwa kuwa wale wanyama wakali kama faru na mbogo wao walikuwa wakifungiwa, na wale wanyama wapole waliachiwa huru, lakini baadaye bustani hii iligeuzwa kuwa pori la akiba (Game Reserve) mwaka 1991 na kupitishwa rasmi kuwa Hifadhi ilipofika mwezi Julai mwaka 2013. Ikiwa na eneo la mita za mraba 0.5, na iko umbali wa km 2 kusini magharibi kutoka katikati ya jiji la Mwanza katika Ghuba ya Ziwa Victoria.
Jinsi ya kufika katika hifadhi hii.
Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane kinafikika kwa njia ya usafiri wa boti ukitokea Mwanza, Mtu anaweza kufika Mwanza kwa gari, ndege au treni na kutoka Mwanza mjini kwakutembea kwa miguu ama kwa gari hadi geti la kuingilia hifadhini.
Shughuli zinazofanyika hifadhini:
Hifadhi ya Kisiwa Cha Saanane inatoa fursa kwa mtalii kuja na kufanya shughuli mbalimbali anapokuwa ndani ya hifadhi pamoja na kuangalia wanyama, kukwea miamba, kutizama ndege, na safari za kutembea, vile vile kupiga makasia.
Turism in Tanzania inakujuza haya mengine kuhusu hifadhi hiyo. Je Wajua!
Hifadhi ya Saanane ni kisiwa chenye madhari mazuri kilichopo ndani ya Ziwa Victoria.
Pia kisiwa kipo karibu sana na jiji la Mwanza ni (Dakika 15 mwendo wa miguu)
Hali kadhalika hii ndio hifadhi ya mwisho kati ya hifadhi zipatikanazo nchini Tanzania, pia ndio hifadhi ndogo nchini Tanzania na Barani Afrika

No comments:
Post a Comment